KERR ASEMA MECHI YA TOTO ITAKUWA NGUMU, LAKINI AFUNIKA HISTORIA
Kocha
Mkuu wa Simba, Dylan Kerr raia wa Uingereza amesema mechi yao dhidi Toto
African kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza itakuwa ngumu
lakini wanachotaka ni pointi tatu.
Kerr
amesema ameelezwa historia ya ugumu wa mechi dhidi ya Toto, lakini kwa
kuwa wanataka pointi tatu, kila kitu watakiacha nyuma.
"Pointi
tatu ndiyo jambo muhimu sana, ushindani ni sehemu ya ligi. Tutaacha
mambo mengine yote ya historia nyuma na kuangalia tunachotaka ambacho ni
pointi tatu.
"Tunajua
mechi ya mwisho wameshinda mabao matano ugenini, hilo linakuwa ni
sehemu ya maandalizi yetu kabla ya kukutana nao," alisema.
Katika
mechi yake ya mwisho, Toto African iliishindilia Majimaji kwa mabao 5-1
ikiwa nyumbani kwao Songea huku Simba ikionyesha kiwango kizuri lakini
ikaambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.
Post a Comment