Wananchi zaidi ya 200 Arusha hawana makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko
Wananchi zaidi ya 200 katika kata
sita wilayani Arumeru mkoani Arusha hawana makazi baada ya nyumba zaidi
ya 60 kusombwa na mafuriko.
Mafuriko hayo ambayo pia yamesomba, Ng’ombe na Mbuzi zaidi ya 50 na
kuku zaidi 120 ya meendelea kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu
ya barabara jambo ambalo limeleta adha kubwa kwa wagonjwa na wajawazito
ambao sasa wanalazimika kubebwa kwa mikono na machela kwenda kupata
huduma.
Viongozi wa vijiji vilivyokumbwa na maafa hayo akiwemo Bw Onesmo
Mollel amesema kuwa wameamua kuwashirikisha wananchi kuanza matengenezo
ya awali katika barabara za mitaa mbalimbali ili ziweze kupitika na
kuimba serikali kwasaidia korofi.
Akizungumza baada ya kutembelea maeneo hayo ya maafa, mkuu wa
wilaya Arumeru Wilsoni Nkhambaku amewataka wote waliojenga maeneo ya
mabondeni pamoja na wale wanaoishi katika mikondo ya maji kuondoka
haraka ili kuepusha maafa zaidi.

Post a Comment