ABRAMOVICH KAMA MAGUFULI, AVAMIA MAZOEZI CHELSEA, AWAELEZA WACHEZAJI ANACHOKITAKA
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ametua katika mazoezi ya timu hiyo kwa kushitukiza.
Mfumo
huo wa kushitukiza ni kama ule unaotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania, John Pombe Magufuli kuvamia sehemu ambayo anaona inahitaji
marekebisho.
Abramovich,
milionea kutokea nchini Russia ametua katika mazoezi ya Chelsea yaliyo
katika eneo la Cobham na kuzungumza na wachezaji huku akiwaambia hakuwa
akitaka kumfukuza Kocha Jose Mourinho, lakini mwisho haikuwa na namna.
Hata hivyo amewaeleza wachezaji hao kwamba huu ni wakati wa kubadilisha mambo na kusaidia timu kurejea katika hali yake.
Abramovich alizungumza kwa lugha ya Kirusi huku wachezaji wakiatafsiriwa alichokuwa akikieleza.
Mazoezi
hayo yalikuwa yakiongozwa na Kocha Steve Holland na Eddie Newton ikiwa
ni kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Sunderland kwenye Uwanja wa
Stamford Bridge, Jumamosi.
Taarifa
za uhakika kwamba Guus Hidink atakuwa kazini lakini ataanza kwa kukaa
jukwaani Jumamosi ili kukiona kikosi hicho kikipambana na Sunderland.












Post a Comment