ad

ad

HADITHI: Msafara wa Mamba - 05


MTUNZI: Ally Mbetu ‘DR AMBE’
...ILIPOISHIA:
Maneno ya Anko niliona sasa yanaelekea kunisimanga, sikutaka kuongeza neno niligeuka na kuondoka. Sikuwa na haja ya kulia japo moyo uliniuma, nilijikaza mtoto wa kike na kurudi hadi nyumbani.
Nilipoingia ndani nilimkuta mama na mwanaume wa kizungu walikuwa wakinywa pombe kali, aliponiona alinyanyuka ili anikumbatie.
"Wawooo..my Babiiii."
Aliponisogelea ili anikumbatie nilimsukuma na kuanguka chini, sikutaka kumuangalia nilikimbilia chumbani kwangu huku nikilia.
SASA ENDELEA…
Mama alinifuata na kuniuliza nalia nini, nilimweleza upuuzi wake wote alioufanya kwa mjomba.
“Najua amekujaza maneno ya uongo, lakini nataka nikupe habari njema mwanangu.”
“Habari gani?” nilimuuliza mama huku nikimtazama macho yaliyojaa machozi.
“Umemuona yule mgeni?”
“Ndiyo mama.”
“Basi yule ni rafiki yangu wa siku nyingi alikuwa amekwenda kwao Ulaya lakini amerudi na kunitafuta na kuniulizia maendeleo yako. Nilimweleza uchungu wako katika elimu, ameahidi kukusomesha mpaka Ulaya.”
“Mama huyu ndiye mwanaume wako wa mwisho au bado una tamaa za mwili?” japo swali lilionesha kukosa adabu lakini ilikuwa lazima nimuulize.
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Anaweza kuwa na nia njema lakini akamtibua kama Anko wa benki.”
“Mwanangu nimechoka kukutia jaka moyo, sasa hivi natulia ili mwanangu nawe upumzike.”
“Mmh! Sawa.”
“Basi njoo umsamilie Anko wako.”
Nilifuta machozi na kutoka hadi sebuleni alipokuwa amekaa Anko mzungu akinywa pombe kali. Alionekana mtu mwenye maono ya mbali kwa jinsi alivyoniuliza na ahadi alizotoa.
“Anko nitashukuru sana.”
“Ni bidii yako tu nikuhakikishia kuyabadili maisha yako ili ije umsaidie mama yako, mama yako kanipa sifa zako hivyo itakuwa kazi nyepesi kukufikisha unapotaka na zaidi.”
“Nitashukuru sana Anko.”
“Jione mwenye bahati katika maisha yako, na kesho tunaanza mipango ya paspoti ili ukimaliza elimu ya sekondari ukasomee chuo Ulaya nchi utakayoichagua na chuo unachokitaka.”
Kwa kweli ilikuwa surprise kubwa kwangu baada ya Anko wa benki kujitoa kunisaidia kwa ajili ya maneno ya mama. Kilichoniumiza moyo ilikuwa tabia ya mama ya kutoridhika na mwanaume mmoja. Niliapa kupambana ili kuibadili tabia yake japo tabia ya mtu ni kama ngozi kuibadili ni kazi kubwa.
Anko mzungu siku ile alilala pale nyumbani huku akiniahidi kumaliza matatizo yaliyokuwa yakitutatiza. Mama alipewa pesa nyingi mbele yangu kwa ajili ya masomo yangu na kumshukuru Mungu kumrudisha mwokozi.
Siku ya pili ilikuwa wiki endi hivyo sikwenda shule, baada ya kufungua kinywa, mama na Anko mzungu walikwenda mjini na kuniacha nyumbani peke yangu nikicheza gemu kwenye laptop ya Anko.
Majira ya mchana Anko mzungu alirudi peke yake nilipomuuliza mama yupo wapi alisema alienda kushughulikia masuala yangu ya paspoti yangu. Baada ya kupumzika alikwenda kwenye friji na kutoa pombe kali na kusogea karibu yangu kwenye kochi na kuanza kunywa.
“ Herena unatumia pombe?”
“Hapana Anko.”
“Hata kidogo.”
“Ndiyo Anko.”
“Jaribu kidogo.”
“Hapana Anko sipendi pombe na nimeapa kutokunywa katika maisha yangu.”
“Mmh! Sawa, basi kachukue juisi kwenye friji ili kila mtu awe na kinywaji.”
Sikutaka kubishana na Anko nilikwenda kwenye friji na kuchukua juisi na kuiweka kwenye glasi na kurudi kuendelea kucheza game.
Nakumbuka kuna kipindi nilikwenda msalani niliporudi niliendelea kucheza game huku nikinywa juisi yangu. Lakini ghafla macho yalianza kupoteza nguvu kama mlevi na Anko alinibeba kunipeleka ndani, baada ya hapo kilichoendelea sikujua.
Nilishtuka usingizini na kujikuta kitandani kwangu, nilijinyanyua kitandani huku kichwa kikiwa kizito, nilipojiangalia nilishtuka kujiona nimeingiliwa kimwili uonesha nimebakwa. Sikuamini hali ile linyanyuka kitandani mwili wote nikihisi maumivu makali.
Nilitoka hadi sebuleni na kuwakuta mama na hawara yake wakiwa wamekumbatiana katika mapenzi mazito. Nilisimama na kuwaangalia kwa muda na kushindwa kuelewa aliyenibaka alikuwa ni yule mzungu au nani.
Nilisimama niliwaangalia huku machozi yakinitoka kwa uchungu, wa kwanza kuniona alikuwa ni hawara ya mama, alinyanyuka na kunifuata nilipokuwa nimesimama na kunivutia kifuani kwake na kuniuliza kwa sauti ya chini.
"Vipi Helena una tatizo gani?"
Sikumjibu nilijitoa mikononi mwake na kurudi nyuma, alipotaka kunisogelea nilimsukuma. Mama alishtuliwa na hali ile na kutaka kujua kwa nini nimekuwa kwenye hali ile. Alinifuata nilipokuwa nimesimama na kutaka kujua kwa nini nipo kwenye hali ile.
"Helana mwanangu mbona kila siku huishi vituko, haya tena una nini?"
"Mama uliyoyataka yamekuwa," nilimjibu mama huku nikilia.
Mama alishtuka na kutaka kunishika, lakini niligeuka na kuelekea chumbani kwangu. Mama alinifuata nyuma hadi chumbani kwangu, nilipofika nilijitupa kitandani na kuanza kulia. Mama alinisogelea ili kujua nina tatizo gani?.
Nilimuelezea mama hali niliyojikuta nayo muda mfupi baada ya kuamka, nilimuonyesha mama hali nilijikutanayo baada ya kuamka, mama hakuamini na kutaka kipi kilichonifanya nilale wakati aliniacha nikijisomea.
Sikumficha nilimweleza jinsi ba mdogo alivyonishawishi kunywa pombe lakini nilikataa na kunywa juisi na baadaye kupoteza kumbukumbu na kujikuta nimelala na nilipozinduka ndipo nilipokuta nimeingiliwa kimwili.
Baada ya maelezo yale na kuona mwenyewe kwa macho yake nilimuona mama akiinama kisha alikuna kichwa na kuniuliza.
"Helena mwanangu unataka kuniambia baada ya kuondoka Anko wako alirudi peke yake?"
"Ndiyo mama, hata mimi nilishangaa lakini sikuwa nalakuhoji."
"Mmh! Sawa, basi leo atanitambua na uzungu wake, pesa zake zisiwe kigezo cha kunibakia mwanangu."
Mama aliyekuwa amekunywa kidogo nilimuona pombe zikimtoka na kujifunga kanga kama anakwenda kucheza mdundiko. Alitoka kama Faru, nami nilimfuata nyuma ili nione mama anataka kufanya nini.
Mama alikwenda hadi alipokuwepo yule mzungu aliyekuwa akiendelea kunywa pombe taratibu. Mama alipofika alimsimamia mbele yule mzungu huku ameshikilia chupa ya pombe kali mkononi.
"Mr Hans amemfanyaje mwanangu?"
"Ooh taratibu, kwani vipi" alijibu yule mzungu huku akinyanyuka kitini kumfuata mama.
"Mr Hans sihitaji kusogelewa ila nataka jibu umemfanyaje mwanangu?" Mama alikuwa mkali na nywele zilimsimama kwa hasira.
Yule mzungu alionesha kutoshtuka na kauli ya mama aliendelea kumsogelea pamoja na kupigwa stop ya kumfuata.
Nilishtushwa na mlio wa chupa kupasuka kwenye kichwa cha mzungu, alikuwa mama aliyempiga chupa iliyompasua vibaya, mzungu alipiga kelele za maumivu.
"Unaniua mama Herena."
"Kufa shetani mkubwa wee," mama kwa hasira alichukua chupa nyingine ya pombe iliyokuwa juu ya meza ili amuyongeze mzungu aliyekuwa ameanguika chini, lakini nilimuwahi ili asimuumize zaidi.
"Mama basi utamuua."
"Wacha afe mshenzi hawezi kunichezea mimi na mwanangu, kwanza kwa kipi hasa?" Mama alikuwa amepandisha hasira.
Nini kitaendelea? Endelea kufuatilia.
Powered by Blogger.