Iyobo akubali kumuachia mtoto mume wa Aunt
MAKUBWA!
Dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo amekubali kuruhusu mtoto
aliyezaa na mwigizaji Aunt Ezekiel achukuliwe na mume wa mwigizaji huyo,
Sunday Demonte aliyeko jijini Abu Dhabi akitumikia kifungo cha msala wa
madawa ya kulevya.
Iyobo
ametoa kauli hiyo mara baada ya Sunday ambaye imeelezwa kuwa anaweza
kutoka wakati wowote kutokana na utii wake gerezani, kutuma salamu kuwa
anafahamu Aunt amezaa na Moze lakini watambue kuwa mtoto huyo ni wake
kwani kitanda hakizai haramu.
“Ameweka
wazi kabisa kuwa kitanda hakizai haramu hivyo Cookie (mtoto wa Aunt)
hawezi kuwafanya watengane, atamchukulia kama mwanaye wa kumzaa kwa
kumpa matunzo yanayostahili,” kilisema chanzo.
Alipoulizwa
Moze kuhusiana na ishu hiyo, alijibu kwa kifupi: “Kama suala ni mtoto
haina shida nitamuachia tu kwani si atapatikana mwingine, siyo ishu
sana.”
CHANZO: GPL
Post a Comment