40 ya Tiffah iliisha huku nyuma ikiacha madeni ya kiasi cha shilingi 1,005,000

OHOOO!
Kuna madai kwamba, ile pati ya kukata na shoka ya kutimiza siku 40 kwa
mtoto wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah
Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliisha huku nyuma ikiacha madeni ya kiasi cha
shilingi 1,005,000, Amani limechimbua.
Ni
siku ya 11 sasa, kampuni iliyopewa tenda ya kupamba kwenye shughuli
hiyo iliyofanyika nyumbani kwa staa huyo, Tegeta-Madale, Dar ya Rachel
Decorations imejipambanua kuwa, inamdai baba Tiffah kiasi hicho cha
fedha na hakuna matumaini ya kulipwa.
MENEJA WA KAMPUNI AZUNGUMZA
Akizungumza na Amani, meneja
wa kampuni hiyo ya mapambo aliyejitaja kwa jina moja la Lutengano
akisema linatosha, alisema wiki moja kabla ya sherehe hiyo iliyokuwa na
mbwembewe nyingi, dada wa Diamond, Esma Platnumz alimtafuta mpambaji
huyo na kumwambia kuwa, kuna tenda.
“Bosi
wangu anaitwa Rachel, ndiye aliyekutana na Esma wakakubaliana kisha
wakaenda kwa Diamond kwa ajili ya makubaliano ya kifedha lakini bajeti
ilikataliwa baada ya kuonekana ndogo na baadaye wakaafikiana kwamba,
afanye kazi kutokana na kiasi cha fedha alichoahidi.
DIAMOND AINGILIA KAZI ZA WATU
“Siku
moja kabla ya tukio (Jumamosi), usiku tulikwenda nyumbani kwa Diamond
(Madale) na vifaa vyetu kwa ajili ya kuanza kazi kwa kuwa shughuli
ilitakiwa kufanyika asubuhi lakini tukiwa katika maandalizi ya kufunga
matenti (turubali), Diamond aliingia na baadaye akatoka, akaanza
kuelekeza anavyotaka kupambwe.
“Tulimweleza
kwamba haiwezekani kutokana na fedha ndogo waliyokuwa wametoa, akaahidi
kwamba yuko tayari kuongeza fedha ilimradi mapambo yaenee kama
anavyotaka na kusema kuwa ana watu wa muhimu watakaofika hapo hivyo
panatakiwa pawe na hadhi zao. Ikabidi tuanze kuchukua vipimo upya,”
alisema meneja huyo.
MAKUBALIANO MAPYA
Lutengano
aliendelea kuliambia Amani kuwa, ilibidi wakubaliane na Diamond upya,
kwamba kama anataka kuongeza sehemu ya mapambo basi gharama ilibidi
iongezeke, akakubaliana na vyote na kutoa fedha kiasi kwa ajili ya
kukamilisha zoezi hilo huku akisema fedha iliyobaki angetoa siku ya
sherehe huku akisema kuwa, mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss
Lady’ alipendelea zaidi makapeti na mito siyo viti kama ilivyokuwa
mwanzo.
“Tukawa
tumekubaliana aongeze shilingi milioni 1,600,000 kwa sababu kulikuwa na
vitu ambavyo vilitakiwa kununuliwa, Diamond alitoa shilingi moilioni
1,300,000 na kubakisha shilingi laki 300,000 lakini pia kabla ya hapo
alikuwa akidaiwa shilingi laki 625,000 kama fedha ya matenti 5 ambapo
kila tenti liligharimu shilingi 125,000.
“Baada
ya matenti yote kufungwa, tukasitisha zoezi la mapambo kuendelea na
mimi siku hiyo sikulala, nikaanza kushughulikia makapeti ambayo Diamond
aliagiza mpaka nikaja kuyapata muda ulikuwa umeshakwenda na hilo
tulishakubaliana kwamba kunaweza kutokea tukacheelewa kwa sababu ya muda
kuwa mbaya akasema yeye anataka iwe hivyo alivyopanga.
Lutengano
anasema baada ya kuzunguka sana Kariakoo, alifanikiwa kupata makapeti
aliyoagizwa na kuyapakia kwenye gari la mizigo kisha kuagiza gari liende
Madale huku yeye akiendelea kutafuta mito na maua.
“Kutokana
na muda ulivyokuwa umekwenda gari lilifika Madale saa 3:00 asubuhi na
wenyeji wakawa wamesusa kwamba vitu vimechelewa, vitu vikashushwa
ikabidi tena mimi nianze kuwaelewesha kwa njia ya simu namna ambavyo
tulikubaliana na Diamond mwenyewe na baadaye vitu vikaandaliwa na
sherehe ikaanza.
“Kwa
kuwa mimi nilikuwa nimechoka, ule muda ambao sasa mtoto ndiyo alikuwa
anatolewa ndani, ikabidi niende kwenye gari langu nikapumzike ili
nisubiri sherehe ikiisha nikaonane na Diamond ili animalizie fedha yangu
iliyobaki ambapo shilingi 625,000 ya matenti, 300,000 ya deni la awali
na 80,000 ya usafiri ambapo jumla ni shilingi 1,005,000.”
MAMA DIAMOND AFUATWA, ASEMA NIVYO SIVYO
“Nikawa
namfuata mama Diamond kumuulizia, akanijibu hovyo kwamba tumewachefua
sana, Esma naye akawa anatukimbia. Nikawaambia watu wangu tuondoke.
“Siku
iliyofuata (Jumatatu) asubuhi nilirudi tena, nikaambiwa Diamond
amesafiri. Cha ajabu mama yake akaniambia hakuna tunachodai na yale
makapeti alinunua mwanaye.
ASHINDA NJE KWA DIAMOND
“Nilikaa
pale nje kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa alasiri. Nikamwambia
amuulize mwanaye kwenye simu ili nijue nini kinandelea, Diamond akajibu
kwa kifupi tena kwa kutuma meseji kwamba si kwa upambaji ule na kusema
kuwa, fedha aliyotupatia anaona inatosha.
“Mimi
nilisema lazima nilipwe fedha zangu, Esma na mama yake wakaniambia mimi
ndiye niwe ninakumbusha mara kwa mara, Diamond ni msahaulifu sana.
Niliondoka, baadaye nilimtafuta meneja wa Diamond (Hamisi Tale ‘Babu
Tale’) kwa sababu Diamond alikuwa hapokei simu yangu,” alisema
Lutengano.
Meneja
huyo aliendelea kusema kuwa, Babu Tale alimjibu yuko bize na bethidei
ya mwanaye lakini baada ya siku chache alimuita akamwambia ameongea na
Diamond akamwambia amemlipa fedha mara mbili lakini hajaridhika na
upambaji wao na fedha aliyoitoa anaona imetosha hivyo hawezi kulipa
zaidi (licha ya makubaliano).
MAMA DIAMOND ASAKWA
Kwa
upande wake, mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ alipotafutwa na
kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kifupi: “Hatudaiwi chochote waulize
haohao waliokupa taarifa na namba zangu (akamalizia na tusi).”
SIMU YA DIAMOND HAIPOKELEWI
Simu ya Diamond ilipopigwa haikupatikana hewani muda wote, lakini Babu Tale yeye alisema hajui lolote kuhusu mapambo.
CHANZO: GPL

Post a Comment