NANI KAMA YANGA HAPA BONGO ANAYENG’AA KIMATAIFA? YAWAPIGA WAZIMBABWE MKONO
NANI kama Yanga hapa Bongo anayeng’aa kimataifa? Naamini wengi
watasema hakuna, ndiyo, kwa sasa hakuna kwa kuwa wameonyesha kuwa
wanaweza kufuta machungu ya Watanzania.

Achana na kipigo walichopata dhidi ya Simba wiki moja iliyopita, achana na malalamiko kuwa Yanga hawakucheza vizuri kwenye mchezo ule, lakini pia sahau kuhusu ushindi mwembamba wa mchezo wa kwanza dhidi ya BDF ya Botswana, jana walionyesha kuwa wenyewe ndiyo vidume nchini kwa sasa; kudadadeki.
Yanga ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, zilianza timu nne sasa wamebaki wenyewe tu baada ya timu nyingine tatu kutolewa kwenye hatua ya awali kwenye Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.Wakiwa hawaaminiki sana, jana waliweza kuichapa Platinum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hakuna anayeweza kukataa kuwa Yanga siyo bora, mabao yote yalikuwa bora na kuwafanya mashabiki kusahau bao la Emmanuel Okwi alilowafunga kwenye mchezo wa Watani wa Jadi wikiendi iliyopita.
Hii ndiyo Yanga, timu iliyopo chini ya kocha Hans van Der Pluijm, hakika kiwango walichoonyesha kinadhihirisha ubora wao.
Yanga walifanikiwa kujipatia bao lao la kwanza kupitia kwa Salum Telela, ambaye alipata pasi safi kutoka kwa Said Juma Makapu na kumchambua kipa wa Platinum ikiwa ni dakika ya 26 tu.
Mashabiki wa Yanga ambao timu yao ilikuwa ikionyesha kiwango cha hali ya juu, waliamka kwa furaha, wakati wakijiuliza nini cha kufanya, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ katika dakika ya 40 aliifungia timu yake bao la pili.
Haruna alifunga bao hilo baada ya Amissi Tambwe, kufanya kazi kubwa kwa kupiga shuti lililomgonga kipa na kumkuta mfungaji aliyefunga kwa ustadi wa hali ya juu.
Baada ya bao hilo, Mbuyu Twite alimkimbilia Niyonzima, akapiga magoti chini, kisha akamfuta kiatu, kuonyesha heshima kutokana na bao hilo. Hata hivyo, pamoja na Yanga kumiliki mpira kwa kiwango cha hali ya juu, mshambuliaji wa Platinum, Walter Musoma, aliwafanya waende mapumziko kwa hofu baada ya kuifungia timu yake bao moja kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 45.
Faulo hiyo ilipigwa kwa ustadi wa hali ya juu, likiwa ni bao la pili anafungwa kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ kutoka nje ya eneo la 18 ndani ya wiki moja.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya hali ya juu, huku Yanga wakitaka kuonyesha kuwa wametumwa na nchi kufanya kazi, katika dakika ya 46, Tambwe alionyesha kuwa yeye ni bora Afrika kwa sasa baada ya kuifungia timu yake bao la tatu akiwahi krosi iliyopigwa na Mrisho Ngassa.
Tambwe raia wa Burundi hili ni bao lake la tatu kwenye michezo mitatu ya Kombe la Shirikisho Afrika, inawezekana Simba wasifurahie rekodi hii kwa kuwa walimtema kwa kile walichodai amekwisha.
Dakika nne tu mbele, mchezaji mwingine ambaye amewahi kuichezea Simba, Mrisho Ngassa, aliifungia timu yake bao la nne, bao hilo lilifungwa baada ya wachezaji wa Yanga kugongeana pasi zaidi ya sita na mpira kumkuta mfungaji aliyeutupia mpira kimiani.
Kutoka hapo mashabiki wa Yanga waliamini kuwa kazi imekwisha na kutawala uwanjani kwa kelele, huku kipa wao Barthez akifanya kazi kubwa sana kuokoa baadhi ya michomo na kuanza kurudisha tena imani.
Wakati mashabiki wakianza kutoka nje, Mrisho Ngassa aliifungia Yanga bao la tano baada ya kuiwahi krosi safi iliyopigwa na Kpah Sherman ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Simon Msuva.
Ngassa na Tambwe kabla ya mechi nyingine za jana, ndiyo walikuwa wakiongoza kwa ufungaji kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, wote wakiwa wana mabao matatu.Ushindi huo wa Yanga, unaifanya timu hiyo icheze mechi sita nyumbani za kimataifa, sawa na dakika 540, bila kufungwa. Mara ya mwisho Yanga kufungwa nyumbani kwenye michuano hiyo ilikuwa ni mwaka 2010 dhidi ya SE Lupopo ya DR Congo.
Baadaye Yanga imecheza dhidi ya Dedebit, Zamalek, Komorozine, Al Ahly, BDF na jana Platinum bila kufungwa nyumbani. Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm alisema: “Nawapongeza wachezaji wangu kwa kufuata maelekezo, wamecheza kama nilivyotaka.”
Kocha wa Platinum, Norman Mapeza, kikosi chake kiligomea chumba cha kubadilishia nguo walichopewa uwanjani hapo na kulazimika kutumia cha waandishi, wakidai walisikia harufu kali kwenye chumba chao.
“Hatukuingia kwenye chumba kwa kuwa kulikuwa na harufu kali sana, hakika tuliona bora tukae huku kwa kuwa kuna hewa ya kutosha,” alisema mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi wa timu hiyo.Mapeza alisema: “Nawapongeza Yanga kwa mtaji mkubwa wa mabao, hakika ni miujiza tu inaweza kutuvusha hapa, wameonyesha kiwango kizuri sana.”
CHANZO: CHAMPIONI JUMATATU

Post a Comment