ad

ad

TAYO WA BBA AKANUSHA KUPEWA $350,000 NA BILIONEA


 
Tayo (kulia) akiwa na mshindi wa BBA 2014 Hotshots, Idris (kushoto).
Mshindi wa pili wa BBA Hotshots, Tayo kutoka Nigeria amekanusha habari zilisambaa wiki hii kuwa amezawadiwa $350,000 na bilionea wa Nigeria, Ayiri Emani baada ya kuzikosa $300,000 za BBA zilizonyakuliwa na Idris wa Tanzania.
Tayo amekanusha habari hizo alipohojiwa na kituo cha Radio 1 South Africa. Amesema kuwa habari hizo za kupewa kiasi hicho kikubwa cha pesa na huku hata hamfahamu bilionea huyo, zimemletea usumbufu kwasababu watu wengi watadhani yeye ni milionea na huku sio kweli.
Tayo aliongeza kuwa yeye na Idris ni marafiki na anatarajia kuja Tanzania mapema iwezekanavyo.
(CHANZO: BIG BROTHER AFRICA 2014)

No comments

Powered by Blogger.