ad

ad

AMISSI TAMBWE ATUA YANGA, SIMBA YAMNASA BEKI HASSAN KESSY


Hayawi Hayawi, Hatimaye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi Tambwe amesaini Yanga.



Tambwe amejiunga na Yanga leo ikiwa ni dakika chache baada ya Simba kumtema.

Mbele ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Francis Kifukwe, Tambwe ameanguka kuitumikia Yanga kwa mwaka mmoja.

Mshambuliaji raia wa Burundi, Amissi Tambwe amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea klabu ya Yanga SC baada ya kutemwa na timu yake ya zamani Simba SC. Tambwe ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita Ligi Kuu Bara baada ya kutupia mabao 19.
Kessy (katikati )akisaini mkataba wa miezi 18 kuichezea Simba SC jana. Kulia ni Geofrey Nyange 'Kaburu' na kushoto ni msimamizi wa Kessy, Athuman Tippo.
Wakati Tambwe akitua Yanga, watani wao Simba SC wamefanikiwa kufunga usajili wake wa dirisha dogo kwa kumsajili beki wa kulia wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhan Kessy aliyesaini mkataba wa miezi 18. 

No comments

Powered by Blogger.