ad

ad

WAANDAMANAJI WAZUA VURUGU MJINI MISSOURI, MAREKANI


Waandamanji wakifurahia jambo baada ya kuchoma maduka wakati wa vurugu hizo.
Polisi wakiwa eneo la tukio kutuliza ghasia zilizotokana na waandamanaji.
Mwanamama huyu akilia baada ya kumwagiwa maji ya kuwasha.
Mmoja wa waandamanaji akiwa na bango.
Mama wa marehemu Michael Brown,  Lesley McSpadden akitulizwa na waandamanaji.
Marehemu Michael Brown enzi za uhai wake.
Polisi aliyempiga risasi Brown, Darren Wilson.
WAANDAMANJI mjini Missouri katika Kitongoji cha St Louis nchini Marekani wamefanya maandamano yaliyoambatana na vurugu usiku wa kuamkia leo baada ya kupitishwa uamuzi wa kutomshtaki polisi aliyemuua kijana mweusi Michael Brown mwezi Agosti mwaka huu.
Polisi mjini humo wamesema vurugu hizo zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko zile za mwezi Agosti baada ya kuuawa kijana huyo.
Brown alifyatuliwa risasi na polisi aitwaye Darren Wilson, Agosti 9 mwaka huu hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka polisi huyo ashtakiwe kwa mauaji.
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa Wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi kuhusu kesi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.