MANCHESTER UNITED YAFANYA KUFURU …TAYARI IMESHAUZA TIKETI 55,000 ZA MSIMU MZIMA OLD TRAFFORD …haijawahi kutokea tangu mwaka 2006
MANCHESTER United imeweka rekodi mpya ya mauzo ya tiketi zake katika ujio wa kocha mpya Louis van Gaal ambapo imeuza tiketi 55,000 za Old Trafford kwa msimu mzima.
Hii maana yake ni kwamba sasa tiketi zilizo wazi kwenye uwanja huo unaochukua watu 76,000 ni 21,000 tu.
Van Gaal anayemalizana na kazi yake ya kuikochi Holland kwenye World Cup ameamsha ari miongoni mwa mashabiki wa Manchester United ambapo mtandao rasmi wa klabu hiyo umethibitsha jana usiku kuwa tiketi 55,000 tayari zimeuzwa Old Trafford kwa kila mechi ya Ligi Kuu mwanzo hadi mwisho wa msimu huu wa 2014/15.
Nafasi hizo 21,000 sasa zimeachwa kwaajili ya mashabiki wa timu za ugenini pamoja na mashabiki wanaochagua mechi za kwenda kuangalia. Hii inakuwa ni mapema zaidi kwa United kufikia mauzo hayo tangu ilipoutanua uwanja wake na kufikia viti 76,000 mwaka 2006.
VIA SALUTI 5 .COM

Post a Comment