ad

ad

Pluijm, Mkwasa wagawana kikosi Yanga

MAKOCHA wa Yanga wamegawana majukumu ya kuiandaa timu ambapo kikosi hicho kimegawanywa katika makundi matatu makuu.

Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa, Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kesho Jumapili jijini Cairo nchini hapa ni lazima wajiimarishe kimbinu.

Pluijm alisema katika maandalizi yao kuanzia jana Ijumaa watakuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku lakini pia yeye atakuwa akiwatengeneza washambuliaji wa kikosi chake huku wasaidizi wake nao akiwapa majukumu ya kufanya.

Kocha huyo alisema Mkwasa atakuwa na kazi ya kuwaandaa mabeki pamoja na viungo wa kikosi hicho na mabeki hawatakiwi kufanya makosa ya kuwaweka ndani ya eneo la 18 washambuliaji wa Ahly huku viungo wakitakiwa kuwa na uamuzi wa kupiga pasi za haraka.

Alisema Pondamali atakuwa na kazi ya kuhakikisha makipa wake hawaruhusu krosi yoyote itakayokuwa katika uwezo wao kuwapita kirahisi, pia wanatakiwa kupiga kelele kuwakumbusha mabeki wao katika majukumu ya ukabaji.

“Mimi nitakuwa nikiangalia umakini wa washambuliaji, bado nataka waongeze umakini katika kusaidia ukabaji, sitaki kuwaona wanatembea,” alisisitiza Pluijm raia wa Uholanzi.
Powered by Blogger.