ZITTO AICHAKAZA CHADEMA LEO HII
MBUNGE wa jimbo la Kigoma mashariki
Zitto Zuberi Kabwe amekigalagaza Chama chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Baada ya kuibuka mshindi katika kesi iliyosomwa na Jaji wa mahakama
kuu John Mtalemwa jijini Dar.
Tukio hilo limetokea mapema leo ambapo
Zito aliwasilisha shauri la kudai mahakama iwazuie kamati kuu ya chadema (CC)
kumjadili kuhusu hatima ya Ubunge wake na kuhusiana na kuvuliwa kwa nyazifa
zake mwishoni mwa mwaka jana
Mahakama kuu imeamua kuwa Zitto
ataendelea kuwa Mwanachama hai wa Chadema mpaka itakamalizika kesi ya awali
inayodai Chadema kumrejeshea nyazifa zake za uongozi ndani ya Chadema ambapo
haki zote za Zitto ndani ya chama chake zitakuwa chini ya uangalizi wa mahakama
mpaka kesi itakapomalizika na kutolewa hukumu
Zitto alifungua kesi ya kudai
kurejeshewa nyazifa zake ambazo alinyang’anywa mwishoni mwa mwaka jana, kesi
hiyo iliambatana na kesi nyingine aliyoifungua hivi karibuni akidai kamati kuu
isimjadili mpaka itakapoisha kesi yake ya awali na leo Mahakama kuu imempa
ushindi Zitto na kuitaka Chadema na kamati zake zote kutomjadili Zitto
Kesi ya Zitto ya awali ya Zitto kudai
nyazifa zake itaunguruma tena mapema februari 13, mwaka huu.
Post a Comment