ad

ad

Tevez aiponda Manchester City.

MILAN,ITALIA
NYOTA wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez,  amesema amehamia Juventus ili kupata ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezaji huyo ametambulishwa mbele ya mashabiki wa Juventus baada ya kusajiliwa rasmi akitokea Manchester City kwa ada ya Pauni 10 milioni.

Tevez mwenye umri wa miaka 29, aliipeleka Manchester City kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili,  lakini amesikitika kwa kuwa wamekuwa wakiondolewa kwenye hatua za awali chini ya kocha wa zamani, Roberto Mancini.

Alisema: “Miaka minne iliyopita niliamua kutoka Manchester United na kutua Manchester City kwa kuwa timu ilikuwa na mipango kabambe.

“Niliona ninaweza kutoa mchango wangu na kufikia malengo, kweli tulitua kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na tukapata ubingwa wa Ligi Kuu England. Sasa naona Juventus ina mipango ya juu zaidi, nadhani ninaweza kuwasaidia.
“Juventus inataka kuendelea kuwa vinara wa Ligi Kuu Italia pia kupata ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.”

Msimu uliopita Tevez alikuwa Mfungaji Bora wa Man City baada ya kupachika mabao 17 kwenye mechi 46, lakini kocha mpya, Manuel Pellegrini, hakutaka kumzuia kuondoka.
Tevez alisema: “Nilizungumza na Pellegrini, nilimwambia nataka kuondoka, hakutaka kunizuia, aliniambia ninaweza kwenda.”
Powered by Blogger.