Moyes amtengenezea ulimbo Bale
LONDON,ENGLAND
HABARI kutoka Manchester United zinasema uongozi
wa klabu hiyo utahamishia mawazo kwa Gareth Bale wa Tottenham iwapo
watashindwa kumnasa, Cristiano Ronaldo, wa Real Madrid.
Kocha mpya wa Manchester United, David Moyes,
ataanza kazi ya kuinoa timu yake keshokutwa Jumatatu na imefahamika kuwa
ataanza mikakati ya kumsajili Ronaldo katika wiki ya kwanza akiwa
kazini.
Lakini kocha huyo anafikiria kumnasa Bale kama mipango ya kumsajili Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 itashindikana. Habari kutoka Hispania zinasema Ronaldo atakutana na viongozi wa ngazi za juu wa Manchester United wiki ijayo.
Hata hivyo suala la kumshawishi kocha mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, ili amuuze mchezaji wake linaonekana kuwa gumu.

Post a Comment