ad

ad

Raia 37 elfu wa J/Afrika ya Kati wakimbilia nchi jirani.


Raia 37 elfu wa J/Afrika ya Kati wakimbilia nchi jirani
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limetangaza kwamba, tangu mwezi Disemba mwaka jana hadi sasa, zaidi ya raia 37 elfu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamelazimika kuyakimbia makazi yao. 

Shirika la Habari la Associated Press limemnukuu msemaji wa shirika hilo Bwana Edrian Edwards akisema kuwa, karibu wakimbizi 31 elfu wamekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku wengine wakikimbilia nchi za Chad na Cameroon. 

Edwards amesema kuwa, wengi wa wakimbizi hao wanakabiliwa na hali mbaya hasa kutokana na kukosa mahitajio muhimu ya kimaisha. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Shirika hilo kwa sasa linajishughulisha na kutoa huduma kwa wakimbizi walioko nchini Kongo na Chad huku wale walioelekea nchi nyengine wakiwa hawajapata msaada wowote.
Powered by Blogger.