MSANII WA BONGO FLAVA 'CHRISS DUNIA' KUTOKA ARUSHA KUWASHIKA MASHABIKI
CHRISS DUNIA
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, maarufu bongo fleva anatarajia kuachia moja kati ya nyimbo zake kali alizorekodi MJ RECORD Dar-es-salaam. Msanii huyo anayetokea jijini Arusha ataachia wimbo wake mmoja kati ya nyimbo 2 alizofanya katika Studio hiyo ya Magwiji wa kuandaa nyimbo zinazobamba zaidi nchini Tanzania na Africa mashariki na kati na Africa kwa ujumla.
Nyimbo hizo
ni TALANTA na mwingine unaokwenda kwa jina la SICHOKI KUKUITA NJOO. Ni nyimbo
kali ambazo Zote zimefanyika MJ RECORD Chini ya Producer Marco Chali, Wimbo huu
wa 2 bado ukiwa bado unaendelea kumaliziwa uko kwenye hatua za mwisho, ndipo
atapima upi auchie wa kwanza.

Fuata link hapa chini kusikiliza wimbo wake wa R. CHUGA
www.2jiachie.com/2013/02/sikiliza-wimbo-wa-rchuga-yetu-wa-criss.html
Picha ya Chriss
Chiss ambae
ana nyimbo kadhaa ambazo zilishasikika kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini
Tanzania na hata nje ya nchi sasa hivi anakuja kivingine akiwa chini ya
usimamizi wa Label ya 2jiachie music
Msanii huyo
anaetokea jiji la Arusha atarajia kuanza kufanya show baada tu ya kuachia
nyimbo hiyo.
Chriss
amewaomba mashabiki wake kuendelea kumpa support na ameahidi kutowaangusha kwa
amerudi kikazi zaidi.
Sikiliza
wimbo wake wa R. CHUGA Hapahapa www.2jiachie.com wimbo aliouimba kama intro wa kuonyesha kwamba yuko fiti na yupo kwenye
game kitambo. Na pia alikuwa na lengo la
kuwaweka sawa mashabiki wake.
Fuata link hapa chini kusikiliza wimbo wake wa R. CHUGA
www.2jiachie.com/2013/02/sikiliza-wimbo-wa-rchuga-yetu-wa-criss.html


Post a Comment