Mastaa wa Afrika wamjia Kanumba Dar
FILAMU ya mwisho kuigizwa na Steven Kanumba Kanumba The Great iliyopewa jina la Love And Power itazinduliwa kwa
aina yake baada ya wasanii kutoka Afrika Magharibi kualikwa.
Mratibu wa tukio hilo, Mosses Mwanyilu, amesema kuwa msanii huyo aliyefariki dunia mwaka jana, alikuwa kipenzi cha wapenda filamu Bongo na nje ya mipaka ya Bongo, hivyo kwa kuliona hilo wameamua kualika wasanii mbalimbali.

Tunatarajia kufanya tukio la kipekee kabisa katika uzinduzi wa
filamu ya Love And Power ya marehemu Kanumba kwa sababu ni mtu wa watu.
Kwa hiyo kutokana na habari ambazo tumekuwa tukizipata kutoka sehemu
mbalimbali, kuna watu ambao bado hawaamini kuwa Kanumba amefariki,
katika kumuenzi tumekusudia kuitendea haki filamu yake, anasema
Mwanyilu.
Filamu hiyo inadaiwa kutabiri kifo cha Kanumba. Katika filamu hiyo pia wapo wasanii kama Irene Paul, Patcho Mwamba, marehemu Sharomilionea na wasanii wengine wengi.
Filamu hiyo inadaiwa kutabiri kifo cha Kanumba. Katika filamu hiyo pia wapo wasanii kama Irene Paul, Patcho Mwamba, marehemu Sharomilionea na wasanii wengine wengi.

Post a Comment