FILAMU YA LOVE AND POWER YA KANUMBA KUINGIA MTAANI RASMI IJUMAA APRILI 12, 2013
Dar es Salaam, 10th April 2013
Imetayarishwa na Kanumba the Great Film, ikiongozwa na Steven C. Kanumba imeandikwa na Ally Yakuti.
Imetayarishwa na Kanumba the Great Film, ikiongozwa na Steven C. Kanumba imeandikwa na Ally Yakuti.
Ile
filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na
wapenzi wengi wa filamu hatimaye mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa
tarehe 12th April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na
kusambazwa nchi nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya
Steps Entertainment Ltd.
Akizingumza na waandishi wa wanahabari
mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa amesema kuwa
“Filamu ya Love & Power ni filamu ya mwisho kutengenezwa na
marehemu The Great Kanumba inaingia sokoni na kuwafikia watanzania wote
siku ya ijumaa,”
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora
iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu Tanzania.
iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu Tanzania.
Akizungumzia kwa ufupi juu ya filamu ya
Love & Power Bwana Myovela, “Filamu ya Love & Power
imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na
Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love
& Power imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania
kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace
Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na
marehemu kuongozwa na Steven Kanumba, Watayarishaji wakuu ni Steps
Entertainment Ltd imetengenezwa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo
tofauti tofauti.
tofauti tofauti.
Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni
Kiswahili lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’.
Umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16 ni filamu nzuri
inayotazamwa na watoto pamoja na familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi
Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Tanzania.
Katika kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao tunaomba kila mdau wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za
kitanzania
kwa kupambana na Maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu, pia tunawaomba
wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps
Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na
kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua filamu ya Love &
Power halali. Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana
na Wasambazaji kwa namba hizi: 0716 788 805, 0713 570 581
Asanteni.

Post a Comment