Usajili wa Drogba wapingwa na klabu yake
Klabu ya Shanghai Shenhua imesema kuwa Didier
Drogba angali mchezaji wake na kuwa uhamisho wake hadi klabu ya
Galatasaray inakiuka masharti ya mkataba wake.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Chelsea, amesaini mkataba wa miezi kumi na minane na
klabu ya Galatasaray inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki.
''Tumeshangazwa sana na tangazo hilo'' Klabu
hiyo ambayo ilimsaini Drogba kwa mkataba wa miaka miwili na nusu mwezi
Julai mwaka uliopita, imesema.
''Drogba angali mchezi wa klabu ya Shanghai Shenhua kwa kuwa mkataba kati yao bado haujakamilika.
Klabu ya Galatasaray siku ya Jumanne ilitangaza
kuwa Drogba atajiunga na klabu hiyo baada ya kukamilika na mashindano ya
kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
Lakini Shenhua imepinga uhamisha huo na kussema
kuwa liko tayari kuwasilisha malalamishi yake ya shirikisho la mchezo wa
soka duniani FIFA.
Mchezaji hiyo mwenye umri wa miaka 34, kwa sasa
yuko nchini Afrika Kusini kuiongoza kikosi cha Ivory Coast katika
mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa na kampuni ya
uhusiano bora inayomuakilisha mchezaji huyo Sports PR Company na
kuchapishwa kwa mtandano wa kijamii wa Twitter, Drogba alisema
anajiandaa kurejea tena katika michuano ya kuwania kombe la klabu binga
barani ulaya kwa mara nyingine.
Galatasaray imefuzu kwa raundi ya muondoana ya kuwania kombe hilo na imepangiwa kucheza na FC Schalke 04 kutoka uUjerumani.
''Hii ni fursa nzuri ya kuichezea timu kubwa na ni nafasi ambayo siwezi kupuuza'' Alisema Drogba.
Shenhua yapata pigo
Wesley sneijder
Agenti wam mchezaji huyo amesema, Drogba
atajiunga la klabu hiyo ya Galatasaray baada ya kukamilika kwa michuano
ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika.
Drogba ni mchezaji wa pili wa hadhi ya juu
kusajiliwa na Galatasaray baada ya Wesley Sneijder aliyejiunga na klabu
hiyo kutoka klabu ya Inter Milan.
Drogba alijiunga na Shanghai Shenhua mwezi juna
mwaka uliopita na ameifunga jumla ya magoli manane baada ya kucheza
mechi kumi na moja.
Awali Drogba alitaka kurejea Ulaya kwa mkopo na klabu yake ya zamani ilikuwa imeanzisha mazungumzo ya kumsajili.
Lakini shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA
lilipinga uhamisho huo, likisema kuwa linakiuka sheria za kimataifa
kuhusu uhamisho na usajili wa wachezaji.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Cheslea Nicolas
Anelka huenda pia anajiandaa kukihama klabu hiyo ya Shenhua, baada ya
kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Juventus.

Post a Comment