Burland akataa kusajiliwa na Cheslea
Jack Butland amekataa fursa ya kujadaliana na Chelsea kuhusu mshahara
wake na masharti ya utendaji kazi baada ya klabu yake kuafiki ombli la
Chelsea la kumsajili kipa huyo wa Uingereza kwa kitita cha pauni milioni
tatu na nusu.
Wiki
iliyopita Birmingham City, ilikiri ipo tayari kwa mazungumzo na klabu
yoyote inayotaka kusajili mchezaji yeyote kutokana na matatizo ya
kifedha.
Lakini, Butland, 19, amekataa fursa hiyo ya
kufanya mazungumzo na Chelsea, akisema nia yake kuu ni kutaka kucheza
mara kwa mara na haoni kuwa Chelsea, itampa nafasi hiyo.
Mmiliki wa Birmingham City Carson yeung
Butland, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza
Uingereza, mwezi Agosti, mwaka uliopita wakati wa mechi yao dhidi ya
Italia ambayo walishinda kwa mabao mawili kwa moja, anataka kusalia na
Birmingham City hadi mwisho wa msimu huu.
Mwezi uliopita, kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo
Peter Pannu, alisema kuwa Birmingham City, huenda ikalazimika kumuuza
mchezaji huyo mwezi huu.
Vilabu vya Southampton na Everton, vilijaribu
kumsajili mchezaji huyo msimu uliopita na pia amehusishwa na vilabu vya
Liverpool, Fulham, Newcastle na Manchester City.

Post a Comment