Kifaa cha Tablet kutoka Afrika
Kifaa cha Tablet kilichoundwa barani Afrika
Simu aina ya smartphone na
kompyuta za tablet zinazosemekana kuwa vifaa vya mawasiliano vya kwanza
kutengenezwa na kampuni ya Afrika zimezinduliwa.
Vifaa hivyo, ambavyo vimebuniwa na mjasiriamali wa Congo,vinatengenezwa nchini China.
Kampuni yake ya VMK, vifaa vyake vinaendeshwa kwa teknolojia ya Android ya Googles.
Kampuni yake ya VMK, vifaa vyake vinaendeshwa kwa teknolojia ya Android ya Googles.
Simu
hizo za smartphone zitauzwa kwa bei ya rejareja ya dola $170, sawa na
pauni za
Uingereza (£105) na kompyuta itauzwa kwa dola $300 sawa na
pauni (£185).
"Ni Waafrika wenyewe, ndiyo watakaofahamu
mahitaji ya Afrika," amesema Bwana Mankou katika mkutano wa Tech4Africa
mjini Johannesburg.
"Apple ni kampuni kubwa Marekani, Samsung ni barani Asia na tunataka VMK kuwa kampuni kubwa barani Afrika."
Kifaa cha Tablet kilichoundwa barani Afrika
Blogu ya teknolojia ya Smartplanet imeripoti
kuwa kompyuta za VMK zinatoa huduma ya uunganishaji wa wi-fi na uwezo wa
gigabytes 4 ambazo zimehifadhiwa ndani yake.
Jina lake, Way-C, lina maana ya "mwanga wa nyota" katika lugha ya Kilingala.
Simu hiyo ya smartphone nyuma na mbele ina kamera na skrini ya ukubwa wa inchi 3.5 sawa na sentimita 8.9.
Verone Mankou, ndiye aliyeunda kifaa hiki
Kuna mipango ya kuuza simu hizi katika nchi kumi za Afrika Magharibi pamoja na Ubelhiji, Ufaransa na India.
Bwana Mankou amesema anatarajia kuzindua uuzaji wa kompyuta za bei nafuu zaidi kwa wanafunzi mwaka ujao.
VMK imesisitiza kuwa wakati bidhaa zake
zinatengenezwa China kwa sababu za unafuu wa gharama, ubunifu na
uhandisi wa simu hizo ni wa Kiafrika.
Hii ni kutokana na baadhi ya watu au kampuni za biashara kupinga uwezo wa kampuni hiyo katika teknolojia ya simu na kompyuta.
Hii ni kutokana na baadhi ya watu au kampuni za biashara kupinga uwezo wa kampuni hiyo katika teknolojia ya simu na kompyuta.
Kampuni ya VMK imesema kinyume na bidhaa
nyingine za awali za simu na komputa zilizosemekana kuwa za Afrika,
bidhaa za VMK hazifanani na bidhaa zozote za aina hiyo katika nchi
nyingine.
Post a Comment