ad

ad

BARCELONA YAITAKA ARSENAL IMSAHAU DAVID VILLA

BARCELONA imewaambia Arsenal wasahau kabisa wazo la kumsajili mshambuliaji David Villa mwezi huu wa Januari.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alikuwa amepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku akiwa amempelela kwa mkopo wa miezi sita West Ham, mshambuliaji wake Marouane Chamakh.

David Villa
Villa, 31 alikuwa akihusishwa kwenda Premier League lakini Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amesisitiza kuwa nyota huyo wa timu ya taifa ya Hispania aliyesajiliwa kutoka Valencia kwa ada ya pauni milioni 31, haendi kokote.
Rosell alisema: “Nathibitisha kuwa hakuna mpango wa kumuuza Villa katika dirisha dogo la usajili,”
“Ni mali yetu na tunamhitaji, bado kuna safari ndefu ya kumalizia msimu.”
Powered by Blogger.