MANCHESTER UNITED KUMTOA WELBECK KWA MKOPO, WAMTAKA ASHLEY COLE
MCHEZAJI wa Manchester United, Danny Welbeck anatakiwa kwa mkopo na timu ya Reading hadi mwisho wa msimu.
Kocha wa United, Alex Ferguson, inaaminika yupo tayari kumwacha kinda huyo akacheze kwa mkopo.
Reading tayari wameshapiga hatua ya kumnasa nyota huyo wa miaka 22.
Wamezidi kuchagizwa na mwitikio wa Manchester United na wanatumai kukamilisha dili hilo mwishoni mwa wiki.
Welbeck ameshindwa kuwemo kwenye mipango ya timu baada ya ujio wa Robin Van Persie.
Pia amekuwa nyuma ya Wayne Rooney na Javie Hernandez.
Wakati
huo huo, Manchester United imeonyesha dhamira ya kumtwaa beki wa
kushoto wa Chelsea, Ashley Cole, ambapo kocha wa United, Alex Ferguson,
amepania kumuunganisha Cole na kiungo wa Chelsea ili wote wawili watue
Old Trafford.
Cole kama ilivyo Lampard, mkataba wake Chelsea unamalizika mwisho mwa msimu.
VIA SALUTI 5
Post a Comment