ad

ad

Muna Love Awataka Wasanii Waokoke


MSANII wa Filamu za Bongo na mdau wa Muziki wa Bongo Fleva, Rose Alphonce ‘Muna Love’ ambaye aliamua kuokoka baada ya mtoto wake, Patrick kuugua na kupona kimiujiza, amewataka wasanii na wadau wake wamrudie Mungu.

Muna aliiambia Full Shangwe kuwa, ataongea na marafiki zake wakiwemo Wakristo na Waislamu wamrudie Mungu kwani kupona kwa mwanaye ni uwezo wa Mungu.

“Ninawaomba marafiki zangu wote wanaonizunguka kumrudia Mungu kwa imani zao. Mimi nimemuona Mungu baada ya kumponya mwanangu kimaajabu. Patrick aliniomba nimuitie mchungaji ili amuombee, nilishangaa kwa imani kali aliyonayo kumbe Mungu aliamua kumtumia ili niokoke.

“Kwa sasa ninaabudu Doricas Ministry iliyoko Kunduchi jijini Dar, ninajipanga kulitangaza neno la Mungu,”alisema Muna.

No comments

Powered by Blogger.