Mbao Yavuruga Sherehe Za Yanga SC Mwaka Mpya
Wachezaji wa timu ya Yanga.
Mbao walicheza kandanda safi jana na kufanikiwa kuwaumbua Yanga kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu Bara, hivyo Jangwani wakaukaribisha mwaka mpya kwa majonzi. Mbao wangeweza kupata bao la tatu baada ya Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kutaka kujifunga. Hii inamaanisha kwamba Yanga haijawahi kupata ushindi dhidi ya Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha timu ya Mbao FC.
Baada ya mechi za kesho (tazama ratiba ukurasa wa nne), ligi itasimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi. Katika mchezo wa jana, mabao ya Mbao yalifungwa na Habib Haji dakika ya 53 na 68. Sasa Haji amefikisha mabao saba ambapo ni bao moja tu nyuma ya kinara wa mabao, Emmanuel Okwi mwenye nane. Katika mchezo huo, David Mwasa alipewa kadi nyekundu (za njano mbili) dakika ya 76 kutokana na kumchezea vibaya Amissi Tambwe wa Yanga.
Katika mchezo mwingine wa ligi jana, Singida United ikiwa ugenini ilishinda 3-0 dhidi ya Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe. Mabao ya Singida yalifungwa na Elinyaieshi Simbi dakika ya 18, Awadhi Salim dakika 43 na Shafik Batambuzi dakika ya 66. Singida imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23.
Stori: Leah Marco, Mwanza
Post a Comment