ad

ad

Kuna Madhara Mwanamke Kumzidi Umri Mpenzi Wake?

BILA shaka msomaji wangu umzima buheri wa afya. Karibu tena kwenye kona yetu hii tunapopeana elimu na maarifa kuhusu suala la uhusiano wa kimapenzi. 


Leo nataka kuzun¬gumza na wanawake ambao wapo kwenye uhusiano na wanaume ambao kiumri ni wadogo kwao.
Imezoeleka kwamba katika uhusiano wowote wa kimapenzi, mwanaume anapaswa kuwa mkubwa kuliko mwanamke, ikitokea mwanamke amemzidi umri mwanaume, basi ataitwa majina yote yasiyofaa, wapo watakaomuita anatoka na ‘serengeti boy’, wengine watasema ‘anambemenda’ na maneno mengine ambayo hayapendezi. 


Inawezekana uhusiano wa aina hii ni mgeni katika mila na desturi za Waaf¬rika lakini utafiti wa kimapenzi unaeleza kwamba, umri si kikwazo katika mapen¬zi. Kuna msemo wa Kingereza usemao ‘age is nothing but numbers’ ukiwa na maana kwamba katika mapenzi, umri si chochote bali ni namba tu.
 

Kama mmependana kwa dha¬ti, tofauti ya umri haiwezi kuwa tatizo kwenu, hata watu wa nje wakizungumza vipi hawawezi kuliathiri penzi lenu kwa saba¬bu mnapendana kwa dhati.
Hata hivyo, z i p o c h a n g a ¬moto am¬bazo mw a n amk e unapoamua k u i n g i a kwe n y e u h u ¬siano na mwanaume ambaye ni mdo¬go kwako kiumri ni lazima uwe tayari kukumbana nazo.
 

1. HESHIMA
Katika mila za Kia¬frika, imezoeleka kwamba mdogo ndiye anayepaswa k u m h e s h i m u mkubwa ku¬liko ambavyo mkubwa anam¬heshimu mdo¬go. Kwamba mdogo ndiye a n a y e p a swa kuanza kumua¬mkia mkubwa wake, anataki¬wa kumsikiliza kwa kila ana¬chomwambia na kuwa na ad¬abu anapokuwa mbele yake. 


Hata hivyo, katika mapenzi huwa ni tofau¬ti, mwanaume ameumbwa kuwa kichwa, hata kama ni mdogo, hulka ya ki¬maumbile, atataka kuheshimiwa, kusiki¬lizwa na kupewa kipaumbele kwa sababu tu ni mwanaume. Na wewe kama mwan¬amke, jukumu lako la kwanza ni kumsiki¬liza na kutii anachokwambia. 


Sasa jiulize, utakuwa tayari kuyafanya hayo kwa mtu uliyemzidi umri? Kama jibu ni ndiyo, basi hilo haliwezi kuwa tatizo ka¬tika uhusiano wenu, mtaishi kwa amani, upendo na uaminifu wa hali ya juu.
 

2. VIKWAZO VYA NDUGU
Ipo wazi kwamba ndugu wa mwanaume, hasa mama na dada zake (mawifi) wa¬napenda kumuona ndugu yao akiingia katika uhusiano na mwanamke ambaye ni mdogo kwake. Wengi wanaamini kwamba ili mwa¬naume awe na mamlaka ka¬mili, ni lazima amuoe mwa¬namke mdo¬go kwake.
I k i t o k e a k w a m b a wewe mwa¬namke ni m k u b w a , maneno na vikwazo vi¬takuwa vingi sana. Itaonekana kama unataka kumfanya ndugu yao ‘mume bwege’, kwamba hata ukiko¬sea atashindwa kukuwa¬jibisha kwa sababu u m e m z i d i umri. 


J i u l i z e k a m a u t a k u w a tayari ku¬kabiliana na kashfa, ma¬tusi na vituko u t a k a v y o ¬kumbana na¬vyo kwa saba¬bu ni lazima vitatokea tu. Kama unad¬hani roho yako ni nyepesi, ni bora ukafiki¬ria uamuzi m w i n g i n e lakini kama ume k u b a l i kujitoa sada¬ka, simamia penzi lako na hakika m t a f i k a mbali licha ya vikwazo hivyo.
I t a e n ¬d e l e a w i k i i j a y o . K w a m a o n i , u s h ¬a u r i , nicheki k w a n a m ¬ba za h a p o juu.

No comments

Powered by Blogger.