WACHACHE WAJITOKEZA MARUDIO UCHAGUZI WA UDIWANI MBWENI, DAR
UCHAGUZI wa marudio ya udiwani katika kata 43 unaofanyika leo sehemu mbalimbali nchini, umeleta hali ya sintofahamu katika Kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam ambako wapiga kura wamejitokeza kwa idadi ndogo kuliko ilivyotegemewa.
Global TV Imefanikiwa kufika Kata ya Mbweni, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kutembelea baadhi ya vituo hivyo ambapo pamoja na hali hiyo, imebaini usalama wa kutosha ambako mawakala na wasimamizi walionekana katika hali ya kuchoka na wengine kupitiwa na usingizi.
Uchunguzi uliofanywa unaonyesha hali hiyo ilitokana na kusubiri wapiga kura ambao walikuwa wakifika hapo mmoja-mmoja baada ya muda mrefu.
Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya wapiga kura waliokuwa wakitegemewa kwenye kata ya Mbweni ni zaidi ya 400 lakini mpaka Global TV inaondoka hapo mchana huu, ni wapiga kura 24 tu waliokuwa wamefika hapo.
NA CATHERINE KAHABI/GPL
Post a Comment