Lissu Awashangaza Watanzania, Picha Zake zaibua Matumaini
Mungu ametenda! Baada ya juzi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Aikael Mbowe kusema kuwa, wananchi wataanza kumuona na kusikia sauti ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, hatimaye picha zake za kwanza zimeonekana akiwa kwenye tabasamu murua hivyo kuwashangaza
wasiojulikana.
Picha hizo zilizosambaa jana kwenye mitandao ya kijamii zilimuonesha Lissu akiwa bado kwenye Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, lakini afya yake ikiwa imetengemaa na kuwa safi kwa asilimia 90.
Picha hizo zilizoteka mitandao ya kijamii ziliibua shangwe na matumaini mapya kwa baadhi ya Watanzania waliokuwa wakikesha kumuombea Lissu alione jua kwa mara nyingine kwa msaada wa Mungu.
“Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa uponyaji wa Lissu kwa kuwa
alilolipanga yeye mwanadamu hawezi kulipangua na amewashangaza wasiojulikana waliokusudia kumuua,” ilisomeka sehemu ya maoni mengi mitandao ambako kila mmoja alikuwa akimrudishia Mungu sifa na utukufu. Katika taarifa yake, Mbowe alisema kuwa, Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alitolewa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na kuhamishiwa chumba cha wagonjwa wa kawaida akiwa na uwezo wa kuongea na kufanya mazoezi. Mbowe alisema kuwa, katika matibabu ya mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, aliwekewa kiasi kikubwa mno cha damu ambapo kwa zaidi ya miaka 20 hakuna mtu aliyewahi kuongezewa damu kiasi hicho hivyo kuweka historia hospitalini hapo.
Mbowe alisema kuwa, baada ya matibabu hayo hospitalini hapo, Lissu atahamishiwa kwenye matibabu katika nchi nyingine ambayo hakutaka kuiweka wazi kutokana na sababu za kiusalama. Lissu alishambuliwa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana, mnamo Septemba 7, mwaka huu nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma ambapo bado polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo. Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wa Chadema aliliambia gazeti hili kuwa, anawashukuru watu wote walioshinda na kukesha wakimuombea Lissu kwani muda siyo mrefu atarejea barabaran
Post a Comment