ad

ad

Famous Furniture Yatua Dar, Wakali Wa Magodoro, Masofa (Video)



KAMPUNI  ya Famous Furniture ya Rochester, New York, Marekani, imefungua duka lake nchini eneo la biashara la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Katika duka lake, miongoni mwa bidhaa kuu zipatikanazo hapo ni pamoja na magodoro na vitanda vya Sealy Posturepedic, sofa na viti vya La-Z-Boy.
  Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) akiongea na muwakilizi wa duka Famous Furniture.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ufunguzi wa duka hilo,  mmoja wa maofisa waandamizi wa kampuni hiyo, Riaan Strydom – Brand Manager, alisema

“Sealy ina uzoefu wa utengenezaji wa magodoro na vitanda kwa zaidi ya miaka 100 na kwa sasa ndiyo chapa inayoongoza kwa kutengeneza vitanda na magodoro bora zaidi duniani kote. Vitanda vya Sealy vimetengenezwa na wataalam wa afya ya mifupa ili kukupatia starehe mfumo bora wa kiafya ili kuhakikisha unapata usingizi mzuri na wenye afya.”
Akifafanua zaidi kuhusu obora wa bidhaa hizo, alisema zaidi ya watu miloni 40 duniani wanapata usingizi mzuri na kuamka wenye afya kwa sababu ya kutumia bdhaa za Seay.


“Tunahakiksha usiku wako unakuwa wenye pumziko na amani. Usingizi mzuri hupoza mwili, unakupa nguvu, unahakikisha unakua vyema na afya nzuri huku akili yako ikizidi kujengeka vizuri. Kumbuka, unatumia theluthi ya maisha yako yote kwenye usingizi. Leo hii, kuna bidhaa mbalimbali za Sealy unazoweza kuchagua lakini lengo letu ni moja; kuhakikisha tunakuwa sababu ya wewe kuwa na maisha yenye starehe.”

Alisema samani za La—Z—Boy zinatengenezwa na kusambazwa kwa leseni katika nchi nyingi duniani.
“La—Z— Boy ina haki miliki za Marekani na kimataifa kwenye miundo zaidi ya 200. Dizaini ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1928 na tangu hapo, wamekuwa ni mabalozi wa  Maisha ya Starehe wanaoongoza duniani,” alisema Dhaesee.

Naye  Ryan Beattie kutoka Bravo Group, msambazaji wa La—Z—Boy kutoka Famous Furniture alisema binadamu hutumia muda mwingi wakiwa wamekaa chini, hii ndiyo ya sababu ya wabunifu, watafiti na wataalamu wa afya kuumiza vichwa kutoa bidhaa zitakazoleta starehe katika mikao.

“Unahitaji kukaa kwenye viti bora na vizuri vinavyokujenga kiafya.  Starehe ya mkao si katika muonekano tu hata aina ya kitu unachokalia kinakupa starehe ya mwili na mfumo bora wa egemezi, hasa kama unakaa kwa muda mrefu,” alisema Beattie.
Kuhusu Famous Furniture Ltd
Famous Furniture Limited (iliyosajiliwa kwa Namba 135127) iliona umuhimu wa kutambulisha bidhaa bora za nyumbani ili kukidhi soko la Tanzania. Bidhaa bora za La-Z-Boy zitaboresha mwonekano wa nyumba yako na starehe yako ya mkao wakati magodoro ya Sealy Posturepedic yatakuhakikishia usingizi wenye afya.
Sasa vyote hivi vinapatikana katika duka namba 47, Mlimani City. Wataalamu wetu wapo tayari kusikia mahitaji yako na kuyafanyia kazi. Famous Furniture inatarajiwa kufungua maduka mengine matano nchini kote kabla ya mwisho wa mwaka 2018.

Famous Furniture ni kampuni iliyo chini ya Bravo Group Manufacturing (Pty) Ltd yenye viwanda saba Afrika Kusini na inayoongoza kwa kuwa na bidhaa bora za chumbani na sebuleni.

No comments

Powered by Blogger.