Uchaguzi Kenya: Odinga Mbishi, Kenyatta Mbabe
Rais Uhuru Kenyatta.
Viongozi hao wameendelea kusisitiza Tume ya Uchaguzi na Mipaka, (IEBC) haiwezi kuaminika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki na wamemtaka mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati kujiuzulu.
Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Rutto wamesema hawatafanya mazungumo na upinzani na uchaguzi lazima ufanyike tarehe 26 Oktoba na wapo tayari.
Pia amewaonya wanaopanga kufanya vurugu kuwashambulia maofisa wa tume na wapiga kura na kusema watadhibitiwa vikali na vyombo vya usalama.
Raila Odinga.
Wakiongea katika mikutano katika Kaunti za Trans Nzoia, Baringo na Laikipia, viongozi hao wa Jubilee wamepuuza wito wa Raila Odinga kujadili mabadiliko katika tume ya uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio
Uhuru Kenyatta alisema, ”Mazungumzo pekee nitakayofanya, nitafanya na Wakenya, wapiga kura ambao nitaomba wanichague. Tume ya Uchaguzi imepewa Ksh. bilioni 12 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi na si kufanya mazungumzo na yeyote.”
Aliongezea pia: ”Nimesikia wanataka kufanya mazungumzo na mimi. Sina muda na mazungumzo hayo, kama Raila hataki uchaguzi anaweza enda nyumbani na kulala na kuwaacha Wakenya watumie haki yao ya kikatiba.


Post a Comment