Wema Sepetu ashindwa kupokea kadi CHADEMA
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani,
Frederick Sumaye, ameahirisha mkutano wa waandishi wa habari
ulioandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi rasmi kadi ya chama hicho aliyekuwa
mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu.
Tukio
hilo lilipangwa kuhitimisha tangazo la wema miezi kadhaa iliyopita
kujiondoa Chama cha Mapinduzi(CCM) na akijiunga na Chadema.
Akizungumza
na waandishi leo wakati akitangaza kuahirisha mkutano huo, Sumaye,
ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu katika awamu ya Tatu, alisema tukio hilo
limeahirishwa kwa sababu Wema ameshindwa kufika kutokana na kubanwa na
ratiba za Mahakama.
"Hadi
sasa Wema yuko ndani ya ukumbi wa mahakama akisubiri kesi yake
inayomkabili, mawakili walitueleza kesi ingemalizika asubuhi na saa 6:00
mchana tungefanya moutano huu,” alifafanua Sumaye.
Wema anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi ambayo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo.
Sumaye
aliyekuwa amengozana na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema
(Bawacha), Halima Mdee na Makongoro Mahanga, alisema Wema angekabidhiwa
kadi na kuzungumza sababu za kujiunga Chadema.
Waandishi
wa habari walifika ofisi za kanda hiyo kuanzia saa 5:00 asubuhi lakini
ilipofika saa 6:00 mchana waandaji wa mkutano huo waliomba kusogeza
mbele muda.
Post a Comment