MSIMU UJAO, TIMU SITA KUPANDA LIGI KUU BARA
SINGIDA UNITED, WAMEPANDA MSIMU HUU. |
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litapandisha
idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19 kutoka 16 za
sasa hadi 20, imefahamika.
Uamuzi
huo umefanyika Jumanne Agosti 22, 2017 wakati Kamati ya Utendaji
inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa
kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Kwa
marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao kutoka Ligi Kuu
ya Vodacom ya sasa ni mbili hivyo kubaki 14. Na ili kufikia timu 20,
timu sita (6) za Ligi Daraja la Kwanza zitapanda daraja.
Kwa
mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la Kwanza, timu, ina maana kwamba
msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi hiyo
ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Makundi ya Daraja, kundi ‘A’ lina timu za African
Lyon, Ashanti United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na
Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na
Polisi Moro ya Morogoro.
Kundi ‘B’ ziko za Coastal
Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market
ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa,
Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.
Kundi ‘C’ lina timu za Alliance School, Pamba na Toto
African
za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma
ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
Post a Comment