Exclusive: Maskini Jini Kabula! Ukimsikia Utalia, Anatia Huruma (Video)
Maskini Jini Kabula! Hali ya kiafya ya msanii wa filamu za Kibongo
aliyepata umaarufu kupitia tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa
'Jini Kabula', inasikitisha na ukipata bahati ya kukutana naye ana kwa
ana unaweza kutokwa na machozi.
Hivi karibu, alitinga kwenye ofisi za Global Tv Online, Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam majira ya usiku ambapo mwandishi wetu alifanya naye mahojiano.
Kilichobainika katika mahojiano hayo, ni kwamba hali ya afya ya akili ya Kabula haipo sawa. Jini Kabula ana tatizo kwenye akili yake na mwenyewe amekiri kwamba ndugu zake walimpeleka Muhimbili ambako alilazwa kwenye wodi ya wagonjwa akili kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kabula anaeleza kwamba hivi sasa hana sehemu ya kuishi, anatangatanga mitaani na ndugu, jamaa na marafiki zake, wamemtenga kutokana na matatizo aliyonayo.
Baada ya mahojiano na Global TV Online, Kabula hakuwa na pa kwenda, hakuwa na sehemu ya kulala, ikabidi waandishi wetu wafuate sheria za nchi zinavyosema kwa kumpeleka Kituo cha Polisi, Oysterbay alikolala mpaka asubuhi ya siku iliyofuatia.
Kama umeguswa na habari hii na unahitaji kumsaidia Kabula kwa chochote, iwe ushauri, makazi au kiuchumi, wasiliana na Global TV Online.

Post a Comment