NEYMAR APIGANA MAZOEZINI BARCELONA NA NELSON SEMEDO, ATIMKA
Mchezaji wa Klabu ya Barcelona, Neymar.
Hali ya mambo ndani ya Klabu ya Barcelona inaonekana haipo sawa baada ya mchezaji wa timu hiyo Neymar kukwaruzana na kushikana na mchezaji mwezake wa timu hiyo.
Neymar amevurugana na beki mpya kikosini hapo Nelson Semedo wakati walipokuwa katika mazoezi ya leo Ijumaa asubuhi. Baada ya tukio hilo, Neymar aliondoka mazoezini hapo wakati programa ikiwa bado haijamalizika. Neymar amekuwa akihusishwa kutua PSG kwa dau la pauni milioni 191, yawezekana tukio hilo likaongeza presha kubwa katika tetesi hizo za uhamisho wake.
Post a Comment