"Mnashindwa hata kutudanganya kwa pipi"- Zitto
Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameuokosoa
mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na
Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo
ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia
Zitto
amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa kumtaka
Waziri Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa apeleke
reli ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine.
"Toka mwaka jana
tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge wemametoa tafsiri
mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni Kigoma Dar es salaam
au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni matawi ya reli ya
kati...... Lakini ujenzi wa 'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita
za awali unatoka Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri
aangalie takwimu ni wapi atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli
nyingine.......Takwimu zinaonesha kwamba mizigo ambayo Tanzania
inahudumia kwa nchi za maziwa makuu ni tani Milioni tano kwa mwaka kwa
mujibu taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2015/2016. Katika hizo asilimia
34 ni Zambia, asilimia 34 ni Kongo, asilimia 12 Rwanda, aslimia 6
Burundi, asilimia 2.6 Uganda...Unapoanza na 'Standard Gauge' matailion
ya fedha ukaipeleka Isaka na Mwanza maana yake ni kwamba unaenda
kuhudumia mizigo aslimia 15 ya mizigo yote tunayoipitisha unaacha kwenda
kuhudumia mizigo asilimia 40 kwa maana ya Kongo na Burundi ambayo yote
inapita Kigoma". Alisema Zitto
Aidha, Zitto amehoji wizara pamoja na
serikali kuwa ni njia gani walizozitama mpaka kuamua kupeleka sehemu
ambayo wanajua haiwezi kuleta faida kwa taifa.
"Economics' gani ambazo
mmetumia katika kuhakikisha kwamba reli inaelekea mahali ambako hakuna
mzigo..Sipendi kusema kwamba Kigoma inatengwa siyo lugha ambayo mimi
kiongozi napenda kuzungumza lakini hili takwimu zote zinaonesha reli
inapaswa kwenda kule ambako kuna faida, hampeleki kule ambako kuna faida
ambako kuna faida hii maana yake nini ?...Lakini siyo hivyo tu Waziri,
kuna fedha za Benki ya Dunia ...kwaajili ya ukarabati wa reli hata hizi
Bilioni 200 za ukarabati wa reli ambao upo sahizi na zenyewe mmepeleka
kule kule mnapopeleka 'Standard Gauge', mnashindwa hata kutudanganya kwa
pipi". Alihoji Zitto
Chanzo: EATV
Chanzo: EATV
Post a Comment