Kampuni ya Sportpesa ya nchini Kenya Yatua Dar Kuidhamini Yanga
Hatimaye kampuni ya kubashiri matokeo, ya Sportpesa ya nchini Kenya, rasmi imetua jijini Dar kuidhamini klabu kongwe ya Yanga.
Kampuni
hiyo itaidhamini Yanga baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyokuwa
yakifanyika kati ya klabu hiyo na uongozi wa Sportpesa.
Sportpesa,
tofauti na Yanga, pia ilikuwa kwenye mazungumzo na vinara wa Ligi Kuu
Bara, Simba ambao nao wanatarajiwa kuingia nao makubaliano.
Kwa
mujibu wa mtandao mmoja wa nchini Kenya, kampuni hiyo imetua nchini kwa
ajili ya kuzindua matawi yake Tanzania na uzinduzi unatarajiwa
kufanyika Mei 9, mwaka huu kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, iliyopo
Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa
kuwa pamoja na kuzindua matawi, pia Sportpesa itapata nafasi ya
kukutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo ya
mwisho kabla ya kuingia mkataba.
“Kwa
heshima na taadhima mnaalikwa katika uzinduzi wa Sportpesa Tanzania
Jumanne ya Mei 9, 2017 katika Ukumbi wa Kibo Ballroom kwenye Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro, Barabara ya Kivukoni,” ilisomeka taarifa kutoka
katika mtandao huo.
Sportpesa
wanakuja Tanzania kuzindua matawi yao, baada ya kuwa katika uwezekano
wa kuidhamini Yanga. Wanaamini kwa kuidhamini Yanga watapata wateja
wengi katika soko la Tanzania.
Wakenya
hao tayari ni wadhamini wa Hull City inayoshiriki Ligi Kuu ya England,
Gor Mahia, AFC Leopards zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, pamoja na klabu
nyingine kadhaa katika soka la Kenya.
Alipotafutwa
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia hilo, alisema: “Yapo
mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika kati yetu na kampuni ambayo yalienda
vizuri, hivyo kwa kifupi tusubirie kidogo hadi mambo yakikamilika
tutaweka wazi.”
Post a Comment