Mbunge Hussein Bashe atumiwa ujumbe wa vitisho kuwa yeye ni miongoni mwa watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya
Mbunge
wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein
Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu
wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.
Bashe
ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma
ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter na Instagram
kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka;
“Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.
"Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. "
Kufuatia
vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali
kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu
wasiojulikana.

Post a Comment