ad

ad

MAN UTD HAITABADILI MSHAHARA WA LUIS NANI

LONDON, ENGLAND
WINGA Luis Nani ameelezwa kuwa hataongezwa mshahara kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka minne, hivyo ana hiyari ya kuondoka ama kubaki Manchester United.
 Staa huyo wa Ureno aliitwa kwenye mkutano wiki iliyopita, na akaelezwa kuwa klabu haitabadili mshahara wake wa pauni 90,000 kwa wiki kwa ajili ya mkataba mwingine wa miaka minne.

Kutokana na ombi lake la kutaka kulipwa pauni 130,000 kukataliwa, sasa staa huyo ana uchaguzi – kuondoka ama kuendelea kubaki Old Trafford, na kama hatasaini mkataba mpya, United itaanza kutafuta mnunuzi na kumuuza mwisho wa msimu.
Nani mwenye miaka 26, alijiunga United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno kwa pauni milioni 14, Julai 2007 na mabosi wa Old Trafford hawataki kuona akiondoka bure atakapomaliza mkataba wake msimu ujao.
Powered by Blogger.