Makonda Aitwa Bungeni Kujieleza......Ni Baada ya Kutoa Kauli za Dharau Dhidi ya Bunge
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya
Kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya
kudharau Bunge.
Maamuzi
hayo ni sehemu ya maazimio manne ya Bunge yaliyopishwa usiku wa kuamkia leo dhidi
ya viongo wanaoteuliwa na Rais hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo
azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI kutoa maelekezo kwa wakuu
wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na
kutoingilia majukumu yasiyo yao.
Hatua
hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita
Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.
Pia
Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa
wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia
majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na
kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,
Alexander Mnyeti.
Baada
ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge,
wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto
Kabwe, Saed Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia
ambapo kwa kiasi kikubwa wote wameoneshwa kukerwa na kauli hiyo
inayodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge
kukamatwa bila utaratibu.
Wakati
mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi
waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho
aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.
Akichangia
mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista
Mhagama amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa
yanayofanywa na viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa
sheria Rais ana majukumu yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu
wao, hivyo kama kuna RC au DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia
Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenye.
Baada
ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo
ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo
hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya Bunge.
Post a Comment