Makonda azijibu tuhuma zilizotolewa na Wema Sepetu kuhusu Masogange
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu
Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake
mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa
kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa
wa madawa ya kulevya.
Akijibu
swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati
akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema,
“Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”
“Hebu
wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana
nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una
taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe
una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena
nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi
hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.
“Kwahiyo
bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu
gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo
sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”
Majina
65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu
ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf
Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.
Post a Comment