Salum Mwalimu awajibu wanaodai kuwa si mkazi wa Kinondoni
Mgombea
ubunge wa Kinondoni kupitia Chadema, Salum Mwalimu amewajibu baadhi ya
watu wanaodai kuwa yeye si mkazi wa wilaya ya Kinondoni, hivyo hana sifa
za kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Akizungumza
leo Januari 22, 2018 katika mahojiano na kituo cha tevisheni cha Azam,
Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar amesema ni
mkazi wa wilaya hiyo na anajua matatizo ya wananchi wake.
“Nilianza
maisha Kinondoni baada ya kumaliza chuo. Nimeishi kwa miaka 14 na niko
Kinondoni kwa miaka zaidi ya 30. Kwa nini Kinondoni? Si kwamba fursa
zimejitosheleza lakini ninaifahamu na ninayajua matatizo ya Kinondoni
kuhusu barabara, afya na elimu.”
Amesema
alipomaliza Chuo Kikuu mwaka 2008 aliishi mtaa wa Togo kisha akahamia
Hananasif, kufafanua kwamba madai kwamba si mkazi wa Kinondoni hazina
ukweli wowote.
Kuhusu
suala la kugombea ubunge akiwa na wadhifa Chadema amesema,
“Ninachotafuta ni uwakilishi wa wananchi, kwa sasa ni mwakilishi ndani
ya chama. Hata CCM kuna wenye vyeo viwili. Tunatafuta mwakilishi
madhubuti ndani ya Bunge na katika chama chetu hakuna changamoto ya
kofia moja au mbili.”
“Kama
ni kofia mbili au moja mbona kuna mawaziri ambao ni wabunge, ili uwe
mbunge ni lazima uwe raia wa Tanzania, lakini mbona Rais John Magufuli
ni mwenyekiti wa CCM, mbona Rais wa Zanzibar ni makamu mwenyekiti wa
CCM, kwa hiyo hilo la vyeo halitupi shida.”
Amesema yeye kiuhalisia ni mzaliwa wa Kikwajuni Zanzibar huku akigusia kwa kifupi kwamba anaungwa mkono na CUF.
Post a Comment