MWASITI AACHIA WIMBO MPYA “KAA NAO” EXCLUSIVELY MKITONI
Moja kati ya wanamuziki wakali na wakongwe wa kike Tanzania Mwasiti ametoa wimbo wake mpya - KAA NAO ambao umeandaliwa na mtayarishaji wa muziki mahiri nchini maarufu kama EMATHE BOY na unaweza kuupakua hapa http://bit.ly/Kaa_Nao
Mwasiti akizungumzia ujio wake mpya amesema “najua mashabiki wangu wamenisubiri kwa muda mrefu sana ila kwa sasa hawatosubiri tena kuanzia sasa
nitatoa nyimbo baada ya nyimbo hivyo nawaomba wakae mkao wa kula na kutoa support kama ambavyo wamekuwa wakinipa muda wote.
KAA NAO – Ni wimbo ambao unamzungumzia mtu ambae yuko kwenye mahusiano lakini mpenzi wake hathamini mapenzi yake kiasi kwamba ina mfanya amwambie
”Kama mapenzi yangu kwako ni adhabu moyo kaa nao”

Post a Comment