MAZOEZI YA MWISHO YA YANGA YA LWANDAMINA KABLA YA KAZI YA WANAJESHI KESHO
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho
leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kabla ya kesho kurejea
na kuanza kazi ya kutetea ubingwa wake.
Yanga chini ya Kocha George Lwandamina
itashuka dimbani kwa mara ya kwanza katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi
ya JKT Ruvu inayomilikiwa na jeshi, kwenye Uwanja wa Uhuru.
Katika mazoezi ya leo, wachezaji wa Yanga walionekana wako fiti na tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili unaonanza kesho.
Post a Comment