Maxence Melo asomewa mashitaka, arudishwa rumande

Mwanzilishi wa mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo asubuhi na kusomewa mashitaka matatu likiwemo la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini.
Shitaka lingine ni kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao.
Kati ya mashitaka hayo matatu, mashtaka mawili amepata dhamana na lakini katika shtaka la 3 amekosa dhamana ambapo kabla hajakamilishiwa dhamana ya shtaka la tatu Melo ameondolewa mahakamani na kupelekwa gereza la Keko.
Taarifa kutoka mahakamani hapo zinadai kuwa wadhamini wa shtaka la tatu walikuwa wamepatikana ndani ya muda lakini upande wa Jamhuri ulikua umeshaondoka.
TAZAMA VIDEO HIZI HAPA CHINI
Post a Comment