FARID MUSSA KIMEELEWEKA, ANAKWENDA ZAKE HISPANIA KUANZA KAZI JANUARI, KAULI YAKE HII HAPA
Klabu
ya Azam, imetangaza kuwa, aliyekuwa kiungo wao mshambuliaji, Farid
Mussa, Januari, mwakani anatarajiwa kujiunga rasmi na Tenerife ya
Hispania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.
Farid
ambaye alitakiwa kujiunga na timu hiyo Agosti, mwaka huu baada ya
kufuzu majaribio, alishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa kibali cha
kufanyia kazi nchini humo ambapo tayari amekipata.
Ofisa
Habari wa Azam FC, Jaffar Idd amesema: “Tunashukuru safari ya Farid
imeiva na rasmi Januari atajiunga na timu yake hiyo mpya kwani tayari
vibali vyote vimekamilika kuanzia visa mpaka kibali cha kufanyia kazi.
“Muda wowote kuanzia leo ataondoka nchini kwenye Hispania kuanza maisha yake mapya, tunamtakia kila la heri huko aendako.”
Naye
Farid alisema: “Nashukuru Mungu kila kitu kimeenda sawa, nitajiunga na
timu yangu mpya Januari, ni jambo jema kwangu kwani ni kwa muda mrefu
nilikuwa nahangaikia kitu hicho tu, lakini sasa hivi kimepatikana.”

Post a Comment