THOMAS MASHALI SASA KUZIKWA KESHO JUMATANO
Mazishi ya bondia Thomas Mashali aliyeuwawa yanatarajia kufanyika keshokutwa jijini Dar es Salaam.
Baba mzazi wa Mashali amesema wameamua kufanya mazishi hayo Jumatano kwa kuwa wanapisha uchunguzi wa polisi.
“Tumewaachia
kidogo polisi wamalizie kazi yao, lakini mazishi yatakuwa Jumatano
badala ya Jumanne kama ilivyokuwa hapo,” alisema.
Msiba wa bondia huyo ambaye ameuwawa na watu wasiojulikana uko kwao Tandale jijini Dar es Salaam.

Post a Comment