Polisi Kutoa Taarifa Ya Kifo Cha Mwanamasumbwi Thomas Mashali Siku Ya Jumatano
JESHI
 la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na 
upelelezi  kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa 
taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.
Akizungumza
 na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi 
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa 
zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu,
 hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.
Kamishina
 Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu 
aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya 
mtaani tu.
“Mimi
 ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa
 niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa 
leo niache tu”alisema Kamishna Sirro.
Post a Comment