EXCLUSIVE MANARA: KIIZA ALIKUWA KIRUSI, MUANZISHA MATATIZO NA ANGEBAKI SIMBA, MIMI NINGEONDOKA
Msemaji
wa Simba, Haji Manara amesema watu wanaweza kushangazwa na Simba
kuwaacha washambuliaji wake wanaong’ara kwenye Ligi Kuu Bara lakini
kumekuwa na sababu tofauti huku akisema Hamisi Kiiza, alikuwa tatizo na
mtengeneza matatizo ndani ya kikosi cha Simba.
Manara amemtaja Kiiza kama chanzo cha matatizo, asiye mvumilivu na mbinafsi kupita wachezaji wote waliowahi kuichezea Simba.
“Kiiza
kweli alifunga mabao 19 kwenye ligi, lakini kwa aina ya uchezaji wa
Simba angefunga hata zaidi ya 25. Lakini tabia yake ni mtu muanzisha
matatizo, ni tatizo kubwa kuliko unavyofikiri.
MANARA |
“Kila
mara alikuwa anaanzisha migogoro, mshahara ukichelewa siku tatu anaanza
kulaumu. Mfano kuna siku nilikwenda mazoezini kwa niaba ya uongozi
kuwaeleza wachezaji kuwa mshahara tayari umeingizwa benki.
“Nikawasubiri
wamemaliza mazoezi, wakaambiwa ninataka kuzungumza naye. Wakati naanza
tu kuzungumza, yeye akarukia na kuanza kusema mishahara leo ni tarehe
tatu, anasikitika sana. Nikamuuliza unajua kilichonileta hapa? Vipi
hausikilizi hata kiongozi anachoongea halafu nawe useme yako.
“Ni
mtu asiye na subira, tukifika hotelini anataka chumba chake kiwe
tofauti na wengine. Anataka achelewe kuja kula, lakini awekewe. Anataka
kwenye basi achelewe, limsubiri. Kwa kifupi ni mtu anayeua morali ya
wachezaji kwa kiwango cha juu kabisa.
“Nikuhakikishie
kama Kiiza angebaki msimu huu, mimi ningeondoka. Maana kungekuwa hakuna
haja ya kupambana halafu ndani ya timu kuna ‘kirusi’ kinawatafuna,”
alisema Manara.
"Kuhusiana na Amissi Tambwe, ukweli ule ulikuwa ni mfumo wa mwalimu Phiri, ilionekana haendani na mfumo naye akaamua aondoke.
"Alikuwa
akimuweka benchi na akiingia hafanyi vizuri hata katika mechi za
kirafiki. Uongozi ulimuamini kocha ndiyo maana ukatekeleza alichosema,"
alisisitiza Manara.
Post a Comment