BRAZIL YATINGA NUSU FAINALI OLIMPIKI, NEYMAR APIGA BAO, AZUA TAFRANI
Neymar
amefunga bao na kuisaidia Brazil kuitwanga Colombia kwa mabao 2-0 na
kutinga nusu fainali ya Michezo ya Olompiki inayofanyika Rio nchini
Brazil.
Neymar ambaye ni nanodha wa Brazil alifunga bao hilo safi kwa mkwaju wa adhabu.
Wakati
fulani mechi hiyo ilisimama baada ya Neymar kumkwatua kwa makusudi
mchezaji wa Colombia. Mwamuzi akamlamba kadi ya njano la wenzake
hawakubali wakataka kumchakaza Neymar, jambo ambalo lilizua tafrani
kubwa.
Brazil lianza kwa kusuasua na kuwafanya mashabiki wake kuanza kuwazomea wachezaji.
Post a Comment